Nov 7, 2014
Oct 29, 2014
Kauli za Bosi Wa YMCMB "Birdman" Kuhusu Beef Ya Drake Na Tyga.
Boss wa Cash Money records Birdman amekaa chini hivi karibuni na kuzungumzia beef ya wasanii wake Drake na Tyga inayopelekea wasanii hawa kutofanya kazi pamoja na kuchukiana.
Birdman anasema
1.Naongea na kubadilishana message na Drake kila siku ila mpaka sasa sijaongea naye kuhusu hili swala.
2] Huwezi kumfananisha Drake na Tyga, Drake ni Drake, namba hazidanganyi, jamaa anauza sana album, hakuna msanii anayefanya anachofanya ikija kwenye swala la kutengeneza muziki bora.
3] Kama Tyga amemdiss Drake kwenye Wimbo wake wa 'Make It Work' ni kawaida kwani Drake anaweza mfanya msanii yeyote amwandikie wimbo.
4] Tyga bado yupo YMCMB Ila sipendi matusi na kejeli zake atabidi afanya maamuzi kama anabaki au anatoka.
NEW AUDIO: Sugu & Professor Jay – Makamanda
Mdau wa Mziki pokea kazi mpya toka kwa wakongwe hawa wawili katika kuihamasisha jamii ya ki TANZANIA kuhusu hali ya sasa na Uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015. Wimbo umefanywa Mwanalizombe Records chini ya Producer Villy.
Oct 27, 2014
Tng All Star Sunday Bonanza
Tng All Star Twenzetu Sunday Bonanza / anza Kustua Ndugu Maujanja Kuyasambaza / muda Ndo Huu Umeshafika Okoa Sanaa / shika Kipaza
Na Kisha Wakilisha Kitaa / Graphic Design / model Mitindo,Artist, Dancers
Djs Na Freestyle Wastue Wana / akuna Malipo Pia Free Kujichanganya.
Eneo la TUKIO NI JENGO LA NASACO zamani ilikuwa MERIDIANI.
kuanzia jumapili ya tarehe 2 / 11 / 2014 saa 8:00 Mchana #Atl
Oct 18, 2014
Mwana FA ft Alikiba. Wimbo mpya ‘Kiboko Yangu’ kuachiwa wiki ijayo
Mwana FA aka Binamu anatarajia kuachia single mpya ‘Kiboko Yangu’, ambayo amemshirikisha Alikiba Ikiwa ni miezi mitano imepita toka aachie ‘Mfalme’.
Binamu ambaye pia anatarajia kupanda kwenye jukwaa la ‘Serengeti Fiesta’ leo (October 18) akiwa na ‘surprises’ kibao, ameiambia Bongo5 kuwa Jumatano ijayo (October 22) single ya ‘Kiboko Yangu’ itakuwa tayari kwenye vituo vya radio.
Kabla hajaachia ‘Mfalme’ May, 2014, Hamis Mwinjuma alikuwa amepanga aanze kutoa ‘Kiboko Yangu’ ambayo ilikuwa tayari imerekodiwa kwenye studio ya MJ Records kabla ya ‘Mfalme’, lakini mipango ilibadilika.
Binamu ambaye pia anatarajia kupanda kwenye jukwaa la ‘Serengeti Fiesta’ leo (October 18) akiwa na ‘surprises’ kibao, ameiambia Bongo5 kuwa Jumatano ijayo (October 22) single ya ‘Kiboko Yangu’ itakuwa tayari kwenye vituo vya radio.
Kabla hajaachia ‘Mfalme’ May, 2014, Hamis Mwinjuma alikuwa amepanga aanze kutoa ‘Kiboko Yangu’ ambayo ilikuwa tayari imerekodiwa kwenye studio ya MJ Records kabla ya ‘Mfalme’, lakini mipango ilibadilika.
Barua ya BASATA kuhusu kibali cha TI na Davido kwenye Fiesta 2014
Nakala iliyopachikwa hapo chini inaonesha barua yenye majibu ya Baraza
la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa Prime TIme Promotions kuhusu maombi ya
kibali cha kumwingiza msanii Clifford Harris (TI) na David Adedeji
Adeleke (Davido) nchini kwa ajili ya tamasha la Fiesta 2014 lililopangwa
kufanyika katika viwanja vya Leaders Club tarehe 18 Oktoba, 2014.
(via ukurasa wa Vinega, Facebook) |
Oct 17, 2014
Hatua na njia za kupata collabo na msanii mkubwa na jinsi ya kupenya soko la US
Meneja wa T.I. na CEO wa Grand Hustle Records, Jason Geter amesema ili msanii wa Afrika aweze kupata collabo na msanii mkubwa wa Marekani, anahitajika kuwa na ushawishi katika sehemu anayokotoka ili awe na kitu cha kumuongezea pia msanii huyo anayetaka kumshirikisha.
Jason Geter
Akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya wadau wa muziki nchini Ijumaa hii, Geter alitolea mfano wa jinsi T.I. alivyokubali kufanya wimbo na P-Square. Alisema alipigiwa simu na rafiki yake aliyemueleza kuwa kundi la P-Square lingetaka kumshirikisha T.I. kwenye wimbo wake lakini bahati mbaya hakuwahi kuwasikia wasanii hao.
“Kiukweli nilikuwa sijawahi kuwasikia kabla, kwasababu Marekani hawachezwi kivile, nina uhakika baadhi ya watu wanawafahamu lakini watu wengi Marekani hawawafahamu kabisa P-Square,” alisema.
Geter alidai baada ya kuambiwa hivyo aliamua kufanya utafiti wake mwenyewe ili kuwafahamu wasanii hao na hivyo aliingia Youtube kuwatazama. “Nilipoenda kufanya utafiti wangu, nikasema wow, hawa jamaa ni wakubwa,” aliongeza.
Alidai baada ya kuona ukubwa wake, aliona kuwa P-Square wana kitu cha kumuongeza T.I.
“Sababu mashabiki wengi wa P-Square wanaweza kuwa hawajawahi hata kumsikia T.I. Kwahiyo hicho ndio kitu cha kwanza kwamba utaenda kumuongezea nini msanii wangu. Msanii wangu ana msingi wa Marekani kukupa, wewe utaweza kumtambulisha kwa kitu kingine?”
Aliongeza kuwa hatua ya pili inahusisha masuala ya fedha na biashara ambapo huusikiliza wimbo anaotaka kushirikishwa msanii huyo. Alisisitiza kuwa mara nyingi suala la fedha au malipo ya collabo sio kitu wanachokiweka mbele zaidi ya kuzingatia kuwa ni nini msanii wake atakipata kutokana na kushirikishwa kwenye wimbo huo.
“Sawa unayo fedha, sasa hatua ya pili, kitu gani unaweza kukioffer kwake, una kitu cha kuoffer kwa msanii wangu? Je wimbo ni mzuri? Kwahiyo hivyo ndio vitu ambavyo unahitaji kuvifikiria. Na mwisho wa siku zote unatakiwa kulinda brand yako.”
Kuhusu njia anayotakiwa msanii kufanikiwa katika soko la muziki wa Marekani, Jason alisema jambo la kwanza ni kuwa na ukaribu na watu kama yeye ambao wana connection na watu wengi pamoja na brands ambazo zimesimama nchini humo. Geter alidai kufanya wimbo na msanii wa Marekani peke yake, haitoshi kwa msanii wa Afrika kufanikiwa kwenye soko la Marekani.
“T.I. alifanya ngoma na P-Square, lakini kiukweli, inahitaji zaidi ya hivyo kupenya soko la Marekani,” alisisitiza Geter. “Inahitaji T.I. na P-Square kwenda kwenye game ya basketball pamoja na kutembea pamoja. Inahitaji uwekezaji huo wa muda kwa msanii wa Afrika kutumia muda kukaa kwenye soko la Marekani.”
Geter alisisitiza kuwa kama msanii anataka kufanikiwa Marekani, anatakiwa kutake risk kwa kuacha fedha nyingi anazopata Afrika na kukubali kupata kidogo Marekani wakati anakuza jina lake. “Kama unaingiza dola 5 Afrika, unaweza kuja Marekani na utakuwa na bahati sana ukipata sehemu sahihi ambazo unaweza ukapata hata dola moja tu. Ni kazi sana kwa watu kuwekeza muda wa aina hiyo na nguvu katika chochote kile, hiyo ndio changamoto kubwa.”
Geter alisema hilo linawezekana kwa kuingia ubia na watu ambao tayari wana nguvu huko kukusaidia.
Kuhusu lugha ambayo msanii anatakiwa kutumia, Geter alisema muhimu ni kufahamu kuongea Kiingereza lakini sio lazima nyimbo ziwe za lugha hiyo kwakuwa muziki unaweza kufanya vizuri hata kama ukiwa umeimbwa kwa lugha nyingine.
“Lakini yote ni kuwa kile ambacho tunafanana ni rhythm. Ni ile beat inayonifanya nicheze na pia hisia ambayo inagusa moyo. So in America to get played on radio and all that stuff, yes you need to know some English but if you got that beat right, we gonna move man.”
Msikilize zaidi hapa,.
Subscribe to:
Posts (Atom)