May 10, 2014

(Official Music Video) AZMA - KUWA NA AZMA

 

Kutoka kwa AZMA:
 AZMA ni lengo, dhumuni au nia,hili ni jina langu kabisa la darasani, na ni jina ambalo nimejiita mwenyewe, wazazi wangu waliniita AZIMA, nikiwa darasa la tatu, nikajibadili na kuanza kujiita AZMA baada ya kuvutiwa na maana ya jina hilo, na nikaanza kuandika AZMA badala ya AZIMA mpaka kwenye daftari la darasani.

KUWA NA AZMA au kuwa na nia,nimeandika huu wimbo kama dedication kwa watu wote,wanao pambana kutafuta maisha, Maisha yana vikwazo sana,tunatapaswa kuwa na AZMA(NIA) ya dhati, katika kufanya jambo lolote, vikwazo ni sehemu ya maisha, tusikate tamaa, kwa kuwa VIKWAZO(challenges) vipo ili kuonyesha ni kiasi gani tuko STRONG.

0 comments:

Post a Comment