STEREO a.k.a B BOY STEREO
Genre: Hip Hop
Ni tangu pale wimbo wa “nitabaki juu” ulivyoanza kusikika kwa hadhira ya Tanzania,stereo akitumia sanaa kuonyesha yeye ni nani.Stereo alianza kufuatilia Hip Hop tangu akiwa darasa la pili, mwaka 1998. Kwa kutambua kuwa ana kipaji cha kufanya Hip Hop mara baada ya kusikia ladha ya huu mziki… hatimaye alianza kuiga kuchana mistari ya emcees wengine wa Bongo, kama vile A.Y., Professor Jay, Complex (R.I.P.), Fid Q ,Solo Thang na Hasheem Dogo Mwendawazimu mpaka ughaibuni kwa kughani nyimbo za Talib Kweli .Xzibit, Jay Z, Notorious BIG, Coolio na Nas.
Stereo alikutana na Nikki Mbishi shule ya msingi, ambapo waliendelea na huo mchezo wa kuimba nyimbo za wasanii wengine.Stereo anadai alianza rasmi kuandika lyrics zake mwenyewe akiwa darasa la nne… pamoja na Nikki.
Akiwa anaonyesha hisia zake kwa kutumia multi-syllable rhymes akipendelea kuokota maneno ya mitaani zaidi, kwa kiasi fulani, hasa yale adimu kama ‘kucheza ndondo’, ‘komando kipensi’, ‘buti lenye uvundo’, ‘msela nondo’, n.k. , mitambao ambayo wengi wanamfananisha na One The Incredible, ambaye pia anapendelea kutumia multi-syllable rhymes.Umoja wao na Nikki Mbishi aliyefanya stereo kupata deal la M-Lab umekuwa ni tochi ya kizazi kipya cha hip hop Tanzania.
Stereo anasomea “bachelor of science in urban and regional planning” huku akiendelea kushika mic na kuiwakilisha mtaa,kwa sasa Stereo yupo chini ya Unity Entertainment kampuni inayomilikiwa na A.y mkataba aliosaini mwishoni mwa mwaka 2012.
Top 5 emcees wa stereo kutoka Bongo, na kwanini?
Professor Jay, Fid Q, Nikki Mbishi, One The Incredible na Kurasa The Page. Jamaa wana mistari na flow kali sana. Sichoki kuwasikiliza kila siku sababu mistari yao inaishi.
Stereo facebook page
kurasa nyingine
tega sikio unaposikianyimbo zake,kama rafiki,nitabaki(juu) na classic ni ushahidi wa kukomaa kwake katika hip hop(click)