Dec 11, 2013

(Photo's):MSANII THE GAME ALIVYOJICHORA TATOO KUBWAAA YA NELSON MANDELA

  
categories: 



game-mandela-tattoo-1

watu wengi duniani wameguswa na kifo cha Mzee Nelson Mandela kutokana na historia yake ya kipekee,kuanzia mataifa ya Asia,Ulaya, Marekani, wanamichezo, waigizaji hadi watu wa kawaida wameonyesha masikitiko yao.
Hii imepelekea msanii nguli wa hiphop The Game ambaye ni mpenzi mkubwa wa tatoo kuonyesha hisia zake kwa kuchora tatoo kubwa za sura za wanae, Barack Obama, Trayvon Martin na Nelson Mandela akiangalia nje ya gereza.
The Game alishea picha akionyesha tatoo hiyo na kuandika 

“The finished ‘Nelson Mandela’ lookin out of the prison bars by @NikkoHurtado done on my side. 7 hour sitting…. Few more hours to tie in the tats around it & we solid,”.

game-mandela-tattoo-2
 
Huyu sio msanii wa kwanza wa hiphop Marekani kuonyesha kuguswa na kifo cha Mzee Mandela, Busta Rhymes ni miongoni mwa walioguswa na kuandika masikitiko yake kwenye twitter, Nicki Minaj pia aliandika alionyesha hisia zake kwa kuandika na akaamua kumalizia kwa maneno matatu ya kiswahili… ‘Madaraka kwa watu’