Aug 5, 2014

Kundi la Rockaz laingia studio, Quick Rocka azungumzia ujio wao

  No comments    
categories: 
Rapper Quick Rocka aka Switcher amesema baada ya kiongozi wa kundi la Rockaz, Chief Rocka kumaliza masomo yake nchini China na kurejea nyumbani, kundi hilo limeingia studio kurekodi nyimbo mpya.
10522783_321302038047755_248808928_n Quick, Chief na Dau Rocka wakiwa studio

Quick amesema wimbo mpya atakaosikika utakuwa wa kundi hilo. “Project inayokuja baada ya Sukido sio ya Quick Rocka tena. Sasa hivi inakuja Rockaz as a crew,” amesema. Hata hivyo rapper huyo amesema katika wimbo mpya wa kundi lao hawatasikika wote. “Single inayofuata ndio tutafanya as a crew wote lakini sasa katika kutengeza misingi na nini tutaanza watu wawili, mimi na Chief.”
Hata hivyo kwenye picha ya Instagram, Quick anaonekana akiwa studio pamoja na Chief na Dau Rocka hali inayoonekana kuwa wanaweza kuwa watatu kwenye wimbo huo.
Rockaz linaundwa na Chief Rocka, Quick Rocka, Mo Rockana Dau Rocka.

0 comments:

Post a Comment