Oct 15, 2014

Snoop Dogg amaliza beef na Iggy Azalea baada ya kushauriwa na T.I

  No comments    
categories: , ,













 
Hatimaye Snoop Dogg amemuomba msamaha rapper wa Australia Iggy Azalea baada ya utani uliozaa beef wiki hii kupitia Twitter na Instagram.
Snoop n Iggy
Snoop alipost clip ya video Instagram siku ya Jumatano October 15 akimuomba msamaha Iggy na kusema amefikia uamuzi huo baada ya kuongea na rapper T.I anayetarajiwa kuwarusha mashabiki wa Tanzania Jumamosi hii pale Leaders club, ambaye ni rafiki wa Iggy na Snoop.
“Boys and girls, I just got off the phone with my boy Tip, the king of Atlanta, and it’s officially over. No more bad talk, I apologize. I apologize. I’m sorry, I won’t do it again,” hayo ni maneno aliyoyazungumza kwenye clip hiyo yenye caption “It’s over I’m bac on my cool s**t no harm no foul. #ifitaintaboutthe much love @troubleman31t respect sorry bout that.”

Iggy hakua na hiyana bali amepokea na kumsamehe Snoop kwa kuandika,

“I appreciate the apology @snoopdogg. Let that be that people, time to focus on the positive things I’ve got going on. no time to dwell on the negative,”
Beef ya wawili hao ilianza siku chache zilizopita baada ya Snoop kumtania Iggy kwa kupost picha ya utani (meme) Instagram inayomwonesha msichana albino na kuandika “Iggy Azalea No Make Up”.

0 comments:

Post a Comment