Oct 15, 2014

Tudd Thomas: Mwaka 2015 utakuwa mgumu na wenye ushindani zaidi kimuziki

  No comments    
categories: ,















 Producer wa ‘Mdogo Mdogo’ ya Diamond, Tudd Thomas amedai kuwa mwaka 2014 ulikuwa mwaka wa mafanikio kwa muziki wa Bongo lakini mwaka ujao utakuwa mgumu kutokana na ushindani ulioanzishwa mwaka huu.
Tuddy Thomas
Akizungumza na Bongo5 jana, Tudd alisema mwaka huu watayarishaji wa muziki wa Tanzania wamefanya kazi kubwa.
“Mwaka huu naufananisha na mwaka 2012, mwaka huu mambo makubwa yamefanyika katika production za muziki hapa bongo. Ukiangalia Man Walter kafanya, Nahreal, Marco Chali, mimi na ma-producer wote wamefanya poa sana. Lakini mwaka ujao ukatua mgumu sana, kila producer atataka afanye kitu ambacho kitamfanya aonekane anastahili. Kwahiyo 2015 ni pasua kichwa sio kwa wasanii pekee hata producers ushindani utakuwa mkubwa sana na huo ushindani ndo utaufanya muziki wetu kwenda mbali zaidi,” alisema Tudd.

Pia Tudd alisema mfumo wake alioanzisha mwaka huu wa kutayarisha nyimbo 5 ama 6 kwa mwaka ni mzuri na utamfanya afanye kazi zake kwa umakini zaidi.
“Kila mtu ana utaratibu wake, mimi kwa mwaka nafanya nyimbo 5 au 6 tu. Huu utaratibu unawapa fursa producers wengine kuonekana. Ukiangalia mwaka huu nyimbo zangu zote nilizofanya ziko vizuri kwenye rotation ya muziki sasa kama ningefanya nyingi zaidi najua kuna watu ningewanyima nafasi kutokana na mimi kuonekana kila sehemu. Pia kufanya nyimbo chache kwa mwaka zinakupa uwezo na nafasi ya kufanya kazi zako kwa utulivu zaidi.”

0 comments:

Post a Comment