Dec 2, 2013

B-Hitz Music Group Wabania Ngoma Zilizoachwa Na Wasanii Ambao Wamejitoa

  
categories: ,



Kutokana na sakata lililotokea hivi karibuni la kutokuelewana na wasanii wake wakubwa watatu; Mabeste, Vanessa Mdee na Gosby na kupelekea kuondoka kwa wasanii hao katika studio  ya B-Hitz.

B-Hitz imechukuwa uamuzi wa kuzuia baadhi ya ngoma zilizokuwa zimebakia za msanii Vanessa Mdee na Gosby, kwa kuwa ngoma hizo ni moja ya project na mali za studio pia, kutokana na mikataba waliyokuwa wamesign wasanii hao.

Uamuzi huo umekuja baada ya wasanii hao kuvunja mikataba yao na kuonyesha utovu wa nidhamu kutokana na kushindwa kuelewana na uongozi wa studio hiyo, ngoma hizo zilizobakia za wasanii hao hazitoruhusiwa kutoka.