Sep 21, 2013

“Tafadhali” Adili Hisabati ft Salu T, Gnako na Rama Dee



Adili Hisabati amewakusanya wakali kadhaa katika ngoma aliyoipa jina la TAFADHALI. Ni ngoma  ambayo ndani inabeba ujumbe unaogusa maisha ya watu. Akiwa na G.Nako, Rama Dee na Salu T  ndani ya hii ngoma wameingiza vitu ambavyo vinamfanya msikilizaji akubali kuwa muda wa michano  real ndo huu...

Salu T ameanza na ujumbe kwa kujiamini akitaka usikie, wengi tunafahamu aina ya muziki wake ambao umesimama katika ukweli na uwazi na si promo za siku hizi. Salu T anasimamisha hiphop elimu nawe tega sikio upate  elimu tosha.

G. Nako hatabiriki na siku zote atakushangaza kwa flow kali!!! na anavyocheza na lugha. Verse yake imejaa punchlines za hatari ambazo yeye ameziwasilisha kwako kwa mtindo wa mahubiri. Huwa napenda kumsikiliza huyu jamaa kwa sababu anamitambao inayokaa kwenye mdundo vizuri.

Adili Hisabati a.k.a Chapakazi anafahamika tangu enzi zile za Choka Mbaya kipindi kile akiwa  Professor Jay na Simple X akiwa na hasira za hii game, Adili wa PEKE YANGU,Adili wa kikazi humu anamaliza verse ya mwisho.....to keep swahili hip hop alive!!!!


Isikilize TAFADHALI upate chakula cha ubongo:.